
Soma au sikiliza nakala inayofuata. Soma au sikiliza tena nakala hii mpaka utakapoifahamu vizuri.
KUTOKA INJILI, TAFSIRI KWA LUGHA NA MILA ZA WASWAHILI
4 Kisha Isa akaongozwa na Roho wa Mwenyezi Mungu kwenda nyikani ili akajaribiwe na ibilisi. 2 Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa.
3 Mjaribu [yaani Ibilis] akamjia na kumwambia, “Ikiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu [yaani wa kiroho], amuru mawe haya yawe mikate.”
4 Lakini Isa akajibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’”
5Ndipo ibilisi akamchukua Isa mpaka mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu [yaani nyumba ya ibada], 6 akamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa: “ ‘Atakuagizia malaika zake, nao watakuchukua mikononi mwao ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’”
7 Isa akamjibu, “Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mwenyezi Mungu wako.’”
8 Kwa mara nyingine, ibilisi akamchukua Isa mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonyesha falme zote za dunia na fahari zake, 9 kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukinisujudia na kuniabudu.”
10Isa akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Mwabudu Bwana Mwenyezi Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’” 11 Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia.
Tumia muda mfupi ukiisimulia tena simulizi kwa maneno yako mwenyewe. Unaweza kuisimulia kwa sauti au kuiandika. Ukiona unahangaika kuikumbuka, isome au uisikilize tena.
Ukiona umeielewa simulizi, uvute ilham. Tumia muda kuifikiria au jadili maswali yafuatayo. Ni vizuri kuyapitia masomo haya pamoja na familia na marafiki zako ili mpate kujifunza na kushirikiana kwa pamoja.
Get Discovery Bible Studies on your phone
Discover copyright ©2015-2026 discoverapp.org
Swahili verses from the Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu). Copyright © 2018 by Biblica, Inc.® All Rights Reserved Worldwide.