Gundua Vitabu Vitakatifu

Somo la 8

Ukombozi: Amri kumi za Mwenyezi Mungu

Surat Kutoka 20:1-21

Isome nakala

Soma au sikiliza nakala inayofuata. Soma au sikiliza tena nakala hii mpaka utakapoifahamu vizuri.

x1.0

Mwenyezi Mungu anamtokezea Musa na kumpa amri zake juu ya mlima wa Sinai.

KUTOKA TAURATI, TAFSIRI KWA LUGHA NA MILA ZA WASWAHILI

20 Ndipo Mungu akasema maneno haya yote:2 “Mimi ndimi Bwana Mwenyezi Mungu wako, niliyekutoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. 3 Usiwe na miungu mingine ila mimi. 4 Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. 5 Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Bwana Mwenyezi Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.

7 Usilitaje bure jina la Bwana Mwenyezi Mungu wako, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure. 8 Ikumbuke siku ya Sabato, uitakase. 9 Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote, 10 lakini siku ya saba ni Sabato kwa Bwana Mwenyezi Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike, wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Kwa kuwa kwa siku sita, Bwana Mwenyezi Mungu aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo Bwana Mwenyezi Mungu akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.

12 Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Bwana Mwenyezi Mungu wako.

13 Usiue.

14 Usizini.

15 Usiibe.

16 Usimshuhudie jirani yako uongo.

17 Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ngʼombe wake au punda wake, wala chochote kile alicho nacho jirani yako.”

18 Watu walipoona ngurumo na radi, na kusikia mlio wa tarumbeta, na kuuona mlima katika moshi, walitetemeka kwa woga. Wakasimama mbali 19 na wakamwambia Musa, “Sema nasi wewe mwenyewe, nasi tutakusikiliza. Lakini usimwache Mungu aseme nasi, la sivyo tutakufa.”

20 Musa akawaambia watu, “Msiogope! Mungu amekuja kuwajaribu, ili kwamba hofu ya Mungu iwakalie, msitende dhambi.” 21 Watu wakabaki mbali, wakati Musa alipolisogelea lile giza nene mahali pale Mungu alipokuwa.

Simulia nakala hii kwa maneno yako

Tumia muda mfupi ukiisimulia tena simulizi kwa maneno yako mwenyewe. Unaweza kuisimulia kwa sauti au kuiandika. Ukiona unahangaika kuikumbuka, isome au uisikilize tena.

Igundue nakala

Ukiona umeielewa simulizi, uvute ilham. Tumia muda kuifikiria au jadili maswali yafuatayo. Ni vizuri kuyapitia masomo haya pamoja na familia na marafiki zako ili mpate kujifunza na kushirikiana kwa pamoja.


Get it on Google Play
Download on the App Store

Get Discovery Bible Studies on your phone

Discover copyright ©2015-2026 discoverapp.org

Swahili verses from the Kiswahili Contemporary Scriptures (Neno: Maandiko Matakatifu). Copyright © 2018 by Biblica, Inc.® All Rights Reserved Worldwide.